Uyui FM
Uyui FM
27 September 2025, 6:46 pm
Na Zabron George
Katika kuadhimisha siku ya Lugha ya Alama Duniani jamii imeshauriwa kuona umuhimu wa kujifunza lugha hiyo ili iweze kusaidia kurahisisha mawasiliano kati ya watu viziwi na wale wasio viziwi.
Wito huo umetolewa na katibu wa chama cha watu wasioona Bahati Sanga wakati akizungumza na UFR ambapo ameongeza kuwa lugha ya alama ni muhimu kwakuwa ndiyo inayotumika kuunganisha jamii hasa kwenye kundi la watu viziwi.

Baadhi ya wakazi wa Tabora wametoa maoni yao juu ya umuhimu wa siku hiyo na kuongeza kuwa luhga hiyo imekuwa msaada katika kukuza mawasiliano hali ambayo inaleta upendo na amani.
Siku ya lugha ya alama Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 23 ikiwa na lengo la kutambua umuhimu wa lugha hiyo katika kusaidia mawasiliano baina ya mtu asiye kiziwi na mtu ambae ni kiziwi.