Uyui FM

Wenza washauriwa kuacha kujirekodi picha za faragha

27 August 2025, 8:26 pm

“Ni vyema jamii ikajikita kuandaa maudhui yatakayo wasaidia kuleta maendeleo”

Kufuatia matukio mbalimbali ya kusambaa kwa picha mjongeo za faragha kwenye mitandao ya kijamii,wenza wametahadharishwa juu ya tabia ya kupiga picha hizo kwani ni kinyume cha sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015.

Zaituni Juma

Wakili wakujitegemea kutoka ofisi ya Makunga law Associete Paul Eugene, amesema  ni vyema jamii ikajikita kuandaa maudhui yatakayo wasaidia kuleta maendeleo.

Wakili Paul Eugene akizungumza na mwandishi wa habari wa Uyui FM Radio
Sauti ya Wakili Paul Eugene

Ameishauri jamii kutenga muda wa kusoma na tambua sheria za nchi.

Sauti ya Wakili Paul Eugene akishauri kuhusu kusoma sheria za nchi.

Baadhi ya wanachi Manispaa ya Tabora wametoa maoni yao  juu ya suala hilo.

Maoni ya wananchi wa Tabora kuhusu picha za faragha

Kwa mjibu wa Wakili  wa kujitegemea Paul Eugene, sheria za makosa ya kimtandao zimefanyiwa marekebisho kwa lengo kuheshimu faragha na kulinda maadili ya kitanzania.