Ofisi za Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Tabora,
Uyui FM

Wananchi Tabora watakiwa kuwabaini wasiojua kusoma na kuandika

20 August 2025, 8:39 pm

Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Tabora, Christopher Boniface Kabalimo akizungumza katika mahojiano maalumu na Uyui FM Radio.

Wilson Makala

Wananchi mkoani Tabora wametakiwa kushirikiana na Serikali kuwabaini watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuwawezesha kupata elimu ya watu wazima na usaidizi wa kitaaluma, hatua itakayoongeza idadi ya watu wenye elimu ya ´K tatu´ yaani kusoma, kuandika na kuhesabu.

Hayo yameelezwa na Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Tabora, Christopher Boniface katika mahojiano maalumu na Uyui FM Radio, Agosti 19, 2025.

Kabalimo amesema kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, mkoa wa Tabora unaongoza kuwa na idadi ya watu wengi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu nchini ikiwa ni takribani watu 1,850,000 sawa na 32% kwa Tanzania nzima, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili kuondokana na changamoto hiyo.

Sauti ya Christopher Boniface Kabalimo akielezea takwimu za wasiojua kusoma mkoani Tabora.

Kwa upande wao wananchi mkoani humo wamepongeza juhudi za serikali katika kuondoa ujinga miongoni mwa Watanzania na kuahidi kutoa ushirikiano kuwabaini watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili wapate elimu hiyo ya watu wazima.

Maoni ya wananchi wa mkoa wa Tabora kuhusu watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.