Uyui FM
Uyui FM
27 January 2025, 2:42 pm

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amewataka wadau wa mahakama kushirikiana kutimiza malengo ya maadhimisho ya wiki ya sheria.
Ametoa wito huo leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria iliyofanyika katika viwanja vya NSSF karibu na TBC Tabora.
Kaimu Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tabora Daktari Mwajuma Kadilu amewasihi wananchi kujitokeza kwenye viwanja hivyo kupata elimu zaidi.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka 2025 nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo.