Uyui FM

Mtibwa Sugar yatamba kufanya vizuri ligi daraja la kwanza

27 January 2025, 1:49 pm

Picha ya kikosi cha Mtibwa Sukari cha msimu wa 2024/25

Klabu ya Mtibwa Sukari imeendelea kufanya vizuri katika muendelezo ligi daraja la kwanza(Championship) kwa kupata matekeo mazuri katika michezo wanayoicheza,Mtibwa sukari inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 41 kwa kushinda michezo kumi na tatu wakisare michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja.

Afisa Habari wa klabu ya Mtibwa Sukari Tobias Kifaru anasema kuwa klabu imeenda tu kutalii katika ligi daraja la kwanza kwani wanaamini kabisa watarejea tena katika Ligi kuu msimu ujao kwani wao wanawachezaji wazuri na benchi la ufundi lililo bora ambalo linaongozwa na kocha Awadhi juma.

Sauti ya Tobias kifaru

Mbali na hivyo Tobias Kifaru amesema kwemba klabu hiyo inawachezaji bora ambao hata timu yao ikipanda daraja msimu wa 2025/26 itahakikisha inawabakisha kwa ajili ya kuendelea kutoa ushindani ulio mkubwa katika ligi kuu.

Sauti ya Tobias Kifaru

Ligi Daraja la kwanza (Championship) ipo katika mzunguko wa pili ambapo timu zote kumi na sita zimecheza michezo kumi na sita hadi sasa huku ushindani ukiwa ni mkubwa katika kuhakikisha timu zinafanya vizuri.

Sbotop