Savvy FM
Savvy FM
August 22, 2025, 2:04 pm

Familia moja iliyopo barabara ya Losaru mtaa wa Bondeni, Kijenge Kusini jijini Arusha imelalamikia utupaji wa taka hovyo na utiririshaji wa maji taka unaofanywa na baadhi ya wapangaji waliopo eneo hilo, hali inayohatarisha afya za wakazi pamoja na usalama wa mazao yanayolimwa katika shamba lao.
Na Jenipha Lazaro.
Wamiliki wa eneo hilo wamesema licha ya kuweka makatazo kwa wapangaji hao, bado utupaji huo wa taka umekuwa ukiendelea mara kwa mara, huku baadhi ya taka hizo zikielekezwa kwenye shamba linalotumika kwa kilimo cha mbogamboga na mazao mengine ya chakula.
Hata hivyo, tumepata wasaa wa kuzungumza na mwenyekiti wa mtaa wa Kijenge Kusini bwana Elias Nicodemus ambaye amekemea vitendo hivyo na kueleza kuwa bado elimu inaendelea kutolewa kwa wakazi ili kudhibiti matukio ya aina hiyo, huku akibainisha kuwa sheria zinaandaliwa kwa lengo la kupunguza na hatimaye kutokomeza kabisa adha hiyo.