Savvy FM
Savvy FM
July 31, 2025, 2:54 pm

Kutokana na ongezeko kubwa la vituo vya kulelea watoto wadogo mchana yaani (day care) katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha huku baadhi ya vituo vingi vikiwa havijasajiliwa nakupelekea serikali chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalumu imeandaa kliniki maalumu ya usajili wa vituo hivyo kwa wilaya zote za mkoa Arusha zoezi ambalo limeanza rasmi hivi karibuni.
Na Jenipha Laazaro
Akitoa taarifa ya uendeshaji wa zoezi hilo Nivoneiya Kikaho Mratibu wa dawati la jinsia na watoto mkoani Arusha ametoa wito kwa wamiliki wa vituo hivyo huku akibainisha baadhi ya nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya usajili huo.
Nao watendaji kutoka wizara ya maendeleo ya jamii ,jinsia ,wanawake na makundi maalumu wamesema kuwa wameona umuhimu kusaidia vituo hivyo kutokana na baadhi ya changamoto zilizoibuliwa na maafisa maendeleo ya jamii ikiwemo uendeshaji wa vituo hivyo bila ya usajili na upatikanaji wa taarifa huku pia mpango huo ukisaidia kuhakikisha usalama wa watoto.
Kwa upande wao wamiliki wa vituo vya kulelea watoto (day care) wamepongeza hatua hiyo ya usajili na kusema kutasaidia kujenga uaminifu kwa wazazi wenye watoto kujitokeza zaidi kuwapeleka watoto wao katika vituo vyao.