Savvy FM
Savvy FM
May 16, 2025, 9:56 am

Wazazi wametakiwa kuwajengea watoto wao uwezo wa kujiamini kutokana na matukio ya kikatili yanayoendelea kushamiri hapa nchini.
Na Mariam Mallya
Afisa Mradi Magdalena Mchome kutoka Taasisi ya (WEGS) inayojihusisha na kuwainua wanawake kiuchumi pamoja na masuala ya kijinsia (WEGS) Iliyopo mkoani Arusha ameyasema hayo wakati akiwa katika studio za Savvy Fm Radio nakusema kuwa ipo haja wazazi kuwajengea kujiamini watoto wao kwani ulinzi wa mtoto unanzaa kwa mtoto mwenyewe.
Afisa huyo ametoa wito kwa jamii kuwalea watoto kwa upendo na kupunguza ukalii na kujenga urafiki pamoja na kuwapa nafasi yakujieleza ili kuweza kutambua/kubaini mwenendo wa tabia za watoto wao.

Kwa upande wake Emmanuel Mwenera Afisa mradi katika Taasisi ya Wegs amezungumzia changamoto zinazopelekea wanawake kushindwa kutimiza ndoto zao ikiwa ni pamoja na mila potofu na ukosefu wa elimu