Radio Kwizera

Jeshi la Magereza Ngara laadhimisha miaka 64

August 23, 2025, 1:39 pm

Baadhi ya askari magereza na viongozi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakiwa katika Hospitali ya Nyamiaga kutoa mahitaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Picha Andrew Nehemia

Matendo hayo ni pamoja na kuchangia damu, kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Nyamiaga.

Na David Mwaluseke- Ngara, Kagera

Katika kuadhimisha miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara baada ya Uhuru, jeshi hilo wilayani Ngara mkoani Kagera limeshiriki matendo ya kijamii katika hospitali ya Nyamiaga wilayani humo.

Matendo hayo ni pamoja na kuchangia damu, kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Nyamiaga.

Baadhi ya Askari magereza wilayani Ngara mkoani Kagera wakifanya Usafi katika hospitali ya Nyamiaga. Picha Andrew Nehemia

Awali Mrakibu wa Jeshi la Magereza wilayani Ngara Moses Sebastian ameeleza kuwa maadhimisho hayo ni kufuatia maelekezo ya Kamishina wa jeshi la Magereza nchini kuruhusu kufanyika ngazi ya wilaya.

Sauti ya Mrakibu wa Jeshi la Magereza wilayani Ngara Moses Sebastian akieleza sababu ya kuaadhimisha miaka 64 ya magereza kiwilaya

Maadhimisho ya miaka 64 ya Jeshi la Magereza Kitaifa yamezinduliwa leo na yatahitimishwa Agosti 26, 2025 huku yakiongozwa na kaulimbiu isemayo Ushirikiano wa Magereza na Jamii kwa urekebishaji wenye tija.