Radio Kwizera
Radio Kwizera
August 22, 2025, 3:56 pm

Kwa kipindi cha miaka minne wasichana hao wamesomeshwa bure na Serikali kupitia mpango wa kuboresha elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-AEP).
Na Shafiru Yusuph- Muleba, Kagera
Wasichana 264 waliokatizwa na masomo ya Sekondari kwa sababu mbalimbali zikiwemo ujauzito wamerudishwa shuleni Mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka minne na kusomeshwa bure na Serikali kupitia mpango wa kuboresha elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-AEP).
Hayo yameelezwa na Mkufunzi Mkazi wa Mkoa wa Kagera kutoka taasisi ya elimu ya watu wazima Bw. Charles Mkwidu, kwenye maonesho ya maadhimisho ya juma la watu wazima kimkoa yaliyofanyika Wilayani Muleba.
Bw. Mkwidu amesema kuwa kwa mwaka 2022 walisomeshwa bure wasichana 92, mwaka 2023 walikuwa 57, mwaka 2023 walikuwa 43 na mwaka huu wa 2025 ni 72.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Simon Chiboni amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii ili kutambua fursa za elimu za watu wazima kupitia Wadau na kutambua mchango wa wadau kupitia taasisi mbalimbali ikiwemo changamoto pamoja na mafanikio.