Vifo vya Wajawazito vyapindukia Kigoma
April 20, 2021, 5:57 pm
Na; Phillemon Golkanus
Serikali ya Mkoani Kigoma imezindua mpango wa dharura wa miaka mitatu unaolenga kukabiliana na vifo vya wajawazito na watoto wachanga vilivyoongezeka hadi asilimia 95 katika vituo vya afya
Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dr Simon Chacha amesema ongezeko hilo limechangiwa na idadi ndogo ya wahudumu wa afya wenye uwezo katika vituo vya kutolea huduma pamoja na miundombinu isiyo rafiki ya kumuwezesha mjamzito kufika kituo cha afya mapema kabla ya kijifungua.
Amesema idadi ya wahudumu wa afya mkoani Kigoma ni Asilimia 33 hali inayosababisha utoaji wa huduma duni na kwamba kila baada ya siku 3 mjamzito mmoja anafariki kutokana na uzazi huku watoto wachanga watatu wakifariki kila siku
Mapambano dhidi ya changamoto hiyo yameanza kwa wadau kutoka mashirika ya kimataifa ikiwemo UNICEF, WHO na UNFPA kwa kuwezesha vitendea kazi ikiwemo Gari la wagonjwa na vifaa vitakavyotumika kuokoa maisha ya mtoto na mama.
Aidha mpango huo wa dharura pia unalenga Kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi, kuongeza wajawazito wanaokwenda Kliniki na Kuongeza idadi ya watoa huduma ngazi ya jamii