Kisa cheje auwawa na kutupwa kando ya bahari
20 February 2023, 13:11 pm
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa mauaji ya mwanaume mmoja aitwaye Abdul Shaa Abdulmajidi mwenye umri wa miaka 47, ambaye amekutwa akiwa amefariki baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu au watu wasiofahamika huku baadhi ya Wananchi wakidai enzi za uhai wake alikuwa anawaingilia Watu kimwili wakiwa wamelala usiku (cheje).
Na Hamza Ally
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa ACP Isack Mushi februari 19, imeeleza kuwa tukio hilo wamelibaini Februari 17, mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kijiji cha Mngoji kata ya Madimba, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Mwanaume huyo amekutwa pembezoni mwa Bahari akiwa na majeraha kwenye mwili wake ambapo yapo madai kwamba Abdul alikuwa anawaingilia Watu wa eneo kimwili bila kujali jinsia kwa njia ya ushirikina wakiwa wamelala usiku ingawa madai hayo hayajathibitishwa amesema Idrisa Ally diwani wa kata ya Dihimba
Mwili wa mwanaume amekutwa pembezoni mwa Bahari akiwa na majeraha kwenye mwili wake.
ACP Mushi amesema uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na Madaktari umebaini kuwa chanzo cha kifo hicho ni kuvuja kwa damu nyingi kutokana na jeraha alilolipata marehemu kichwani baada ya kupigwa.
Jeshi la polisi linaendelea kuchunguza sababu za mauaji hayo na halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wahalifu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na uvunjifu wa Amani amefafanua ACP Mushi
Jeshi la polisi linachunguza sababu za mauaji hayo na halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wahalifu wote watakaobainika.