Mzee Mkuchika aiomba serikali daraja kilambo kuinganisha Mtwara na Msumbiji
16 February 2023, 10:55 am
Waziri wa nchi ofisi rais kazi maalum Kapteni mstaafu George huruma Mkuchika akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara mkoani Mtwara, kilichofanyika katika ukumbi wa Boma ameiomba serikali kutengeneza daraja katika mto Ruvuma ili kuunganisha mkoa wa Mtwara na nchi jirani ya Msumbiji.
Na Abdullah Abeid
Teyari kuna daraja kaatika mto Ruvuma linalounganisha Mtwara na nchi ya Msumbiji maeneo ya Mtambaswala lakini huko ni mbali na mji wa Mtwara wenye fursa nyingi kama bandari na kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote lakini maeneo haya ya mji wa Mtwara pia yapo karibu na miji mikubwa katika nchi ya Msumbiji hivyo daraja linahitajika katika maeneo ya Kilambo ambayo yapo karibu na mji wa Mtwara.
Tunaiomba serikali ianze kufikiria kujenga daraja pale Kilambo badala ya pantoni tupate daraja, mi nina uhakika Dangote angekua anapeleka saruji nyingi sana huko.
Mzee Mkuchika
Swala la daraja katika mto Ruvuma maeneo ya Kilambo ni jambo amabalo limekuwa likielezwa mara kwa mara na mbunge wa jimbo la Mtwara Mh Hassan Mtenga.