Hekima na busara, sababu ya amani msimbati
31 January 2023, 12:23 pm
Jaji Mfawidhi wa Makahama Kuu ya Kanda ya Mtwara Mhe.Zainab Muruke amemtaja mzee Issa Mohamed Mkumba kuwa ni kinara wa kutatua changamoto za migogoro katika jamii bila kufikishana katika vyombo vya usuluhishi na Mahakama.
Na Hamza Ally
Mzee Mkumba amekua akijitolea kusuluhisha migogoro ya wananchi katika kata ya Msimbati yenye vitongoji 16 vya vijiji jirani vya Mtandi, Ruvula na Mmiyo vyenye wakazi 9,351 kutokana na sensa ya mwaka 2022.
Jaji Muruke amesema mzee huyo amekuwa akitumia hekima na busara alizopewa na Mwenyezi Mungu kutatua migogoro kutokana na kurithi kipaji cha usuluhishaji kutoka kwa babu yake ambaye aliongozana naye kwenye shughuli hizo.
mzee huyo amekuwa akitumia hekima na busara alizopewa na Mwenyezi Mungu kutatua migogoro kutokana na kurithi kipaji cha usuluhishaji kutoka kwa babu yake ambaye aliongozana naye kwenye shughuli hizo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Mtwara