Upakiaji makaa ya mawe Mtwara
Radio Ahmadiyya

Bandari Mtwara inavyokabiliana na vumbi la makaa ya mawe

13 December 2022, 11:14 am

na Mc Kaluta

Upakiaji makaa ya mawe Mtwara

Upakiaji makaa ya mawe Mtwara

Mizinga sita ya kumwaga maji (Misty Cannon Sprayer) imefungwa katika bandari ya Mtwara ili kudhibiti vumbi la makaa ya mawe kutoka katika maeneo hayo. Lakini pia magari ya kumwaga maji na kunyonya vumbi yanafanyakazi kutwa nzima ili kudhibiti kabisa vumbi la Makaa ya mawe.

Kaimu meneja wa bandari ya Mtwara Bw Nobert Kalembwe anaeleza zaidi ya tani laki nane za makaa ya mawe zimeshasafirishwa na bandari ya Mtwara kupitia meli 19. Na mipango yao ni kujenga bandari maalum kwaajili ya kusafirisha mizigo michafu kama haya Makaa ya mawe.
#BandariMtwara