Mamcu & Tanecu zarejesha kwa jamii
7 February 2023, 13:31 pm
Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao cha Masasi, Mtwara Cooperative Union (MAMCU) na Tandahimba, Newala Cooperative Union (TANECU) vimetoa Gawio la Shilingi Milioni 253 kuchangia utatuzi wa changamoto zilizopo katika sekta za Elimu, Maji na Afya kwa mkoa wa Mtwara.
Na Asia Kilambwanda
MAMCU ambao wanahudumia wakulima wa Wilaya za Masasi, Mtwara na Nanyumbu, wametoa Milioni 203, huku TANECU kinachohudumia wakulima wa wilaya za Tandahimba na Newala wakitoa Milioni 50.
Mwwnyekiti wa MAMCU Siraji Mtenguka, alitoa mchanganuo wa fedha hizo kuwa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya mfuko wa elimu, Milioni 75 za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya za Nanyumbu, Masasi na Mtwara.
Huku Milioni 60 kwa ajili ya afya kwa wilaya hizo zote Tatu za maeneo ambako MAMCU wamekuwa wakihudumia wakulima wao, lakini pia shilingi milioni 18 kwaajili ya ujenzi wa visima.
Haya yote tunayafanya kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali ambazo zinafanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan, tunaona juhudi zake anazozifanya hasa katika sekta nzima ya kilimo anatupatia pembejeo bure.
Biadia Matipa-Meneja wa MAMCU
Naye mwenyekiti wa TANECU Karimu Chipola alieleza maendeleo katika sekta ya elimu ambayo yanachangiwa na msaada unatoka kwao vyama vikuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, amevipongeza vyama hivyo kwa kutoa sehemu ya mapato yao na kurudisha kwa jamii.
Kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu, viwango vikubwa vya ufaulu vilivyoonekana nilikua napitia kwenye group sijui ni la wadau wa elimu au sijiu la tunaifungua Mtwara kuna mtu mmoja kaposti kwamba katika wilaya yangu sina zero.
Kanali Ahmed Abbas