Apatikana akiwa amefariki eneo la mpakani
30 January 2023, 12:32 pm
Na: Hamza Ally
Taarifa za awali zinadai kuwa mwili wa Elvida Anael maarufu kwa jina la Mama Chamicha, ambaye ni mstaafu wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani idara ya Mifugo toka mwaka 2020, umekutwa maeneo ya mpakani mwa Mkoa wa Mtwara na Lindi.
Mtoto wa Mama Chamicha, Jesca Chamicha amekiri kupokea taarifa za mwili wa mamaake kukutwa katika eneo hilo la mpakani.
Mapema jana Januari 29, 2023, kwenye makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp yanayohusisha zaidi wakazi wa Mtwara, ulisambaa ujumbe ulioambatana na picha yake, ukieleza mazingira yakutoweka nyumbani kwake mtaa wa Nandope jirani na Hoteli ya Laville Barabara ya Triple V kata ya Rahaleo ambapo inadaiwa alifika nyumbani kwake majira ya asubuhi Januari 28 akirejea toka sokoni akiambatana na mwanamke ambaye hakufahamika kabla ya kuondoka tena ghafla na hakupatikana tena.