Radio Ahmadiyya

Aondolewa kwenye makazi baada ya miaka 24

7 February 2023, 11:58 am

Chuno manispaa ya Mtwara Mikindani.

Na Zainabu Jambia

Uongozi wa Serikali ya mtaa wa Namtibwili kata ya Chuno manispaa ya Mtwara- Mikindani, mkoani Mtwara umesikitishwa na kitendo kilichofanywa na kampuni moja ya udalali iliyotajwa kwa jina la Adili, kuiondoa kwa nguvu kwenye nyumba familia ya mwanamke mmoja aitwaye Pendo Liumba kwa madai kuwa eneo lililojengwa nyumba hiyo limemilikishwa kwa mfanyabiashara katika manispaa hiyo huku kesi ya kupinga umilikishwaji ikiwa bado inaendelea mahakamani.

Akizungumzia kuhusu kutokea kwa tukio Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa amesema kitendo hiko ni unyanyasaji na uvunjifu wa sheria kwa kuwa ni utaratibu wa serikali kushirikisha viongozi wa ngazi za chini kwenye utekelezaji wa shughuli mbalimbali, sambamba na kukiuka taratibu za mahakama.

Cheche Ally

Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Namtibwili