Habari za Jumla
22 March 2021, 5:24 am
Kikwete asema Tanzania ipo salama mikononi mwa Rais Samia
Na; Mariam Kasawa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh.Jakaya Kikwete amesema Taifa la Tanzania lipo salama chini ya uongozi wa Rais mpya Samia Suluhu, kwani rais huyo anafahamu kile kilicho fanyika Tanzania, kinachostahili kufanyika pamoja na mipango ya Serikali…
21 March 2021, 1:57 pm
Hatimaye zoezi la kumuaga Dkt John Magufuli lahamia Dodoma
Na; Mariam Kasawa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani wametakiwa kujitokeza mapema katika uwanja wa Jamhuri kwaajili ya kushiriki zoezi la kumuaga hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassani…
21 March 2021, 11:57 am
Zoezi la maandalizi lakamilika Jamhuri
Na; Mariam Kasawa Zoezi la kuandaa uwanja wa Jamhuri kwaajili ya kuupokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mpaka sasa yamekwisha kamilika . Akizungumza na vyombo vya habari Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Patrobas Katambi amesema…
21 March 2021, 11:39 am
Tubadirike Magufuli kurudi Kilosa hatopita barabara wala Reli ya mwendokasi .
Waumini wa Romani katoliki parokia ya familia takatifu Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wametakiwa kubadirika ndani ya mioyo yao na kumrudia Mungu hasa kipindi hiki cha kwaresma kwa kufunga Kulia na kuomboleza kwakuwa hakuna anaejua siku wala saa ya kifo chake…
21 March 2021, 10:30 am
Marais wa nchi 10 kumuaga Magufuli Dodoma
Na ; Mariam Kasawa. Marais zaidi ya 10 wa Mataifa mbalimbali Duniani wamethibitisha kuhudhuria shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli itakayofanyika kesho mjini Dodoma. Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abasi amesema hadi sasa ana orodha…
21 March 2021, 9:51 am
viongozi wa Jeshi wakagua mandalizi ya kumuaga Rais Hayati Magufuli Dodoma
Na; Mariam kasawa Viongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamekagua ujenzi wa banda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuupokea na kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri…
20 March 2021, 4:05 pm
Waadvendista wasabato wafanya matendo ya huruma -Kilosa.
Waumini wa Kanisa la Waadvendista wasabato Kilosa lililoko Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wameadhimisha wiki ya huduma kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma kama vile kuchangia damu , kutoa mahitaji kwa watu wenye mahitaji maalumu , ikiwa ni pamoja na…
20 March 2021, 3:13 pm
Ratiba ya kumuaga Hayati Dr, John Pombe Magufuli Mkoani Dodoma
Na; Rabiamen Shoo. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kumuaga Hayati Dr. John Pombe Magufuli kutokana na mengi aliyo yafanya katika mkoa huu ikiwemo kuhamishia makao makuu mjini hapa. Akizungumza na…
20 March 2021, 11:41 am
Chuo kikuu Dodoma (UDOM) waikumbuka misingi iliyo jengwa na Rais Magufuli
Na, Mariam Kasawa. Wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma ( UDOM) wamesema wanatarajia misingi imara katika Elimu iliyo wekwa na Hayati rais Dkt John Pombe Magufuli itaendelea kuimarika. Wakizungumza na Dodoma fm wanafunzi hao wamesema wamepokea msiba huu kwa majonzi makubwa…
20 March 2021, 10:11 am
Simanzi na Vilio vyatanda jijini Dar es salaam
Na, Mariam Kasawa. Maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na viongozi wastaafu wa Serikali zilizopita wamefika Uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais…