Vwawa FM Radio

BOT yatoa agizo kuhusu utunzaji wa noti

August 13, 2025, 7:11 pm

Leo ni kutaka zidumu kwa muda mrefu zikiwa safi. Picha na Mtandao

Na Mwandishi wetu

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imewasihi Wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu kuzitunza vizuri fedha aina ya noti ili kutekeleza sheria za nchi.

Meneja Msaidizi idara ya uchumi na takwimu wa BOT, Dkt Ulrick Mumburi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Vwawa Fm jijini Mbeya.

Dkt Mumburi amesema utengenezaji wa fedha unatumia gharama kubwa na kwamba ni jukumu la kila mtanzania kuzitunza fedha halali za noti na hata sarafu.

Sauti ya Dkt Ulrick Mumburi 1

Aidha Meneja Msaidizi huyo amezungumzia pia  umuhimu wa kuzitambua alama zote kwenye noti ili kuepuka mkenge wa kupokea noti bandia.

Dkt Mumburi amesema ni jambo la muhimu kwa kila Mtanzania kuzitambua alama 11 zilizopo kwenye noti ili kuepuka kupokea noti bandia ambayo ni kosa kisheria ukikutwa nayo.

Sauti ya Dkt Ulrick Mumburi 2