Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
June 1, 2025, 11:20 am

Kanisa la Last Church of Tanzania limeendesha zoezi la kugawa misaada ya bidhaa muhimu kwa wahitaji wilayani Mbozi, likisisitiza kuwa huduma hiyo itaendelea kila mwezi.
Na Anyisile Fredy
Askofu wa Kanisa la Last Church of Tanzania, David Sichone, amesema utoaji wa msaada kwa wahitaji ni sehemu ya utume wa kiroho wa kanisa hilo, akisisitiza kuwa huduma hiyo itaendelea kila mwezi na wanafanya hivyo kama maandiko yasemavyo
Mmoja wa walionufaika, Bi. Sifa Munjwanga, amesema msaada huo umekuja kwa wakati sahihi na kuleta faraja kwao. Ameongeza kuwa matukio kama haya yanawapa matumaini mapya.
Msaada huo ni ishara ya upendo na mshikamano wa kidini, ukiibua hamasa ya kuwasaidia wenye uhitaji bila kujali tofauti za kiimani.