Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
May 7, 2025, 12:46 pm

Malengo ni kupunguza ndoa kuvunjika
Na Pili Mwang’osi
TAASISI zinazofungisha ndoa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, zimewataka wanandoa hususan vijana kuwa wavumilivu ili kupunguza wimbi la ndoa kuvunjika.
Ofisa Tarafa ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Edward Lugongo , ametoa wito huo alipozungumza na Vwawa FM Mei 6, 2025. Lugongo amesema wanandoa wanapaswa kuvumiliana kutokana na ukweli kwamba kila mmoja ana madhaifu.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Vwawa, Iku Mwakisimba amezungumzia moja ya chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.
Mchungaji Iku ametoa wito kwa wanandoa kupenda mafundisho pamoja na kufuata kanuni za Mungu kuhusu ndoa huku akisisitiza vijana kuacha tamaa
Aidha naye Mwinjilisti wa kanisa hilo Ambwene Mwanyerere na katibu wa wanawake kanisa la EAGT Sayuni wametoa maoni yao.