Uyui FM

Ligi kuu daraja la kwanza mpira wa pete yaanza kitaifa Tabora

27 September 2025, 5:50 pm

Na Kimwaga Shaban

Mashindano ya ligi kuu Daraja la kwanza Taifa ya mchezo wa Pete ambayo yanafanyika katika Mkoa wa Tabora kuanzia Jumamosi Septemba 26, 2025  katika viwanja vya shule ya  Tabora wasichana (Tabora Girls).

Akizungumza na UFR Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Pete Mkoa wa Tabora Bi. Maimuna Abbas amesema mashindano hayo ni makubwa kufanyika katika mkoa wa Tabora pia ameahidi kuukuza mchezo huo katika Mkoa huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Pete Mkoa wa Tabora Bi. Maimuna Abbas Akizungumza na UFR
Sauti ya Bi. Maimuna Abbas

Kwa upande wa katibu wa wa chama hicho Mwalimu Mwajuma Yusuph amesema hadi sasa maandalizi kwa upande wa Mkoa yamefikia hatua za mwisho lakini amewatoa shaka washiriki wote kuwa hadi ifikapo jioni ya leo kila kitu kitakuwa kimekamilika kwa asilimia mia.

Mwalimu Mwajuma Yusuph katika mahojiano na UFR
Sauti ya Mwalimu Mwajuma Yusuph

Mashindano hayo yanazikutanisha timu 15 kutoka katika mikoa mbalinbali huku mkoa wa Tabora ukiwa na timu mbili kutoka katika wilaya ya kaliua na Nzega.