Uyui FM

CCM Tabora wasema uteuzi wa wagombea ulifuata haki

27 August 2025, 8:16 pm

Zaituni Juma

Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tabora kimewataka wanachama kutambua kuwa, mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya udiwani na ubunge ni wa haki na hauna upendeleo.

Katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Tabora IDDY MAMBO amesema hayo leo wakati akizungumza na UFR juu ya nafasi ya ‘’wajumbe’’ katika mchakato wa kura za maoni kuwachagua wagombea.

Katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Tabora IDDY MAMBO akielezea mchakato wa uteuzi wa wagombea.
Sauti ya Iddy Mambo

Kwa upande wake, katibu wa CCM wilaya ya Tabora Daniel Mhina amesema, wana imani kubwa na mgombea alioteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya ubunge.

Katibu wa CCM wilaya ya Tabora Daniel Mhina akimnadi mgombea wa Ubunge Hawa Mwaifunga.
Sauti ya Daniel Mhina

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Tabora mjini Hawa Mwaifunga, amesisitiza umoja miongoni mwa wanachama.

Sauti ya Hawa Mwaifunga
Mgombea Ubunge jimbo la Tabora mjini CCM, Hawa Mwaifunga

Chama cha mapinduzi CCM kimefanya uteuzi wa mwisho wa majina ya wanachama walioomba nafasi za ubunge na ujumbe wa baraza la wawakilishi wa jimbo na viti maalumu Agost 23 mwaka huu.