Uyui FM
Uyui FM
27 August 2025, 7:50 pm

“Jeshi limejipanga kuwadhibiti watakao kiuka sheria na taratibu katika kipindi cha kampeni“
Zaituni Juma
Jeshi la polisi mkoa wa Tabora limejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi la kampeni kuelekea uchaguzi mkuu linafanyika kwa amani na utulivu.
Akizungumza na UFR Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Richard Abwao amesema, jeshi hilo limejipanga kuwadhibiti watakao kiuka sheria na taratibu katika kipindi cha kampeni.
Kamanda Abwao amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu.
Badhi ya wananchi wametoa rai kwa jamii kushiriki kampeni kwa amani na kusikiliza Sera za wagombea ili kupata kiongozi bora.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kampeni zinatarajia kuanza mnamo Agosti 28 hadi Oktoba 28 mwaka huu.