Uyui FM
Uyui FM
21 July 2025, 6:56 pm

”Hakuna mazingira yoyote ya utekaji ni tukio la ajali” SACP Abwao
Zaituni Juma.
Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limesema kuwa kifo cha mtoto wa miaka mitatu Ramin Sahibad ni tukio la ajali na sio utekaji, ambalo limetokea baada ya kutumbukia kwenye kisima kilichopo nyumbani kwao eneo la Malabi kata ya Mpera Manispaa ya Tabora.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Richard Abwao amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mkuu wa wilaya ya Tabora Upendo Wella ametoa rai kwa wananchi kuweka uzio na kufunika visima kwenye maeneo wanayoishi ili kuepuka madhara ya vifo kwa watoto.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wazazi na walezi kuwa waangalifu na kuhakikisha watoto wao hawachezi karibu na visima, sambamba na kuwataka wamiliki wa visima kuhakikisha wanaweka uzio au kufunikwa kwa usalama wa jamii husika.