Uyui FM
Uyui FM
14 June 2025, 10:19 am

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amekabidhi trekta hizo kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ikiwa ni katika kutimiza ahadi aliyoitoa chuoni hapo.
Na Zaituni Juma
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha amekabidhi trekta mbili (2) kwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika tarehe 10 Juni, 2025 chuoni hapo.
Makabidhiano hayo ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyoahidi tarehe 23 Novemba, 2024 alipohudhuria mahafali ya kumi (10) ya chuo hicho ili kuchangia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mkuu wa Chuo cha AMUCTA, Profesa Juvenalis Asantemungu amesema trekta hizo zitatumika katika kuandaa mashamba darasa kwa ajili ya wanafunzi wa chuo hicho.

Lengo la Wizara ya Kilimo na serikali ni kuchangia uendelezaji wa mafunzo kwa vitendo katika sekta ya kilimo na kuongeza soko la ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu nchini.
