Unyanja FM

Nyasa watakiwa kuzingatia sheria

January 3, 2026, 2:35 pm

Pichani ni Mtangazaji wa Unyanja FM akizungumza na Msimamizi wa Elimu jamii,Kamanda Jastine Ally Athumani katika studio ya Unyanja FM.

Wananchi Wilayani Nyasa wameaswa kuepuka makosa na uvunjaji wa sheria mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu.

( NA:  Said Mlelwa )

Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Elimu jamii, Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyasa, Kamanda Jastine A. Athumani wakati akizungumza katika kipindi Maalumu kupitia Unyanja Fm ambapo ameeleza kuwa Wananchi wanapaswa kujiepusha na makosa, mihemko na ajali mbalimbali ambazo mara nyingi zimekuwa zikisababishwa na Madereva boda boda, baadhi ya  Wananchi kutokana na Ulevi, Wivu wa kimapenzi pamoja na ugomvi mwingineo huku akitaja maeneo ya Fukwe mbalimbali kutokana na mwingiliano wa wageni wengi wanaochanganyika na wenyeji.

Pichani ni Kamanda Jastine Athumani akizungumza katika studio ya Unyanja FM

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Wilayani humo likishughulikia kata zaidi ya Ishirini limeendelea kujipanga vema na kutoa elimu zinazoambatana na Ziara, Vipindi Maalumu sambamba na Oparesheni zinazofanyika ili kuhakikisha usalama na Sheria zinazingatiwa vema.