Unyanja FM

Siku ya afya ya akili duniani Dkt. Hokololo atoa somo

10 October 2025, 9:54 am

Kwenye picha ni Dkt. Hokororo mtalamu wa Afya ya Akili kutoka hospitali ya wilaya ya Nyasa

Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Masuala ya kiafya ya akili na Saikolojia, Dkt. Hokololo akizungumza na Unyanja Fm katika kipindi maalumu ambapo amesema kuwa kitakwimu inaonesha tukio hilo linakua zaidi kwani katika kundi la watu saba mtu mmoja ni muathirika wa tukio hilo hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari.

Ikiwa ni katika siku ya kuadhimisha siku ya Afya ya akili duniani siku ya leo, Oktoba 10 wananchi wameaswa kuepukana na visababishi vya tatizo hilo ili kujijenga vizuri kiafya.

Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Masuala ya kiafya ya akili na Saikolojia, Dkt. Hokololo akizungumza na Unyanja Fm katika kipindi maalumu ambapo amesema kuwa kitakwimu inaonesha tukio hilo linakua zaidi kwani katika kundi la watu saba mtu mmoja ni muathirika wa tukio hilo hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari.

Aidha, Dkt. Huyo ameongeza kuwa ziko njia ambazo watu wanaweza kuzitumia ili kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo Kujitambua katika uwezo wa kiuchumi, kujifunza bila kikomo, kufanya kazi kwa bidii ili kulinda utimamu sambamba na kuwa na mchango chanya katika jamii kuanzia ngazi ya familia, kazi na jamii kwa ujumla.

Akizungumza juu ya waathirika wakubwa wa Afya ya Akili, Dkt huyo amesema kuwa Waajiriwa wanaathirika zaidi kutokana na mzunguko wa mahusiano ya kikazi sambamba na mfumo wa maisha ya kijamii hivyo wanapaswa kuwa wawazi katika changamoto, kuishi vema na jamii na kutafuta suruhisho katika changamoto hizo.

Ikumbukwe kuwa, maadhimisho ya Afya ya akili duniani yalianza rasmi mnamo mwaka 1992 yakidhamiria kuwakumbusha wanajamii juu ya kujikinga na vyanzo vya tatizo hilo na kwa mwaka huu 2025 yanabebwa na kauli mbiu isemayo “upatikanaji wa huduma ya afya ya akili wakati wa Majanga na dharula”.