Unyanja FM

Viongozi wa shule wapewa mafunzo ya manunuzi

September 11, 2023, 9:46 am

Afisa manunuzi wilaya ya Nyasa akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka shule za msingi na sekondari,[picha na,Sichali Netho Afisa habari wilaya ya nyasa

Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani Nyasa wapatiwa mafunzo kuhusu manunuzi ya umma.

Na Sichali Netho

Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Septemba 9, 2023 imetoa mafunzo ya mfumo wa manunuzi wa umma (NeST) kwa wataalam kutoka shule za msingi, sekondari na afya.

Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo jinsi ya kuandaa mpango wa manunuzi kutoka katika idara zao.

Mafunzo yanafanyika shule ya msingi Kilosa Kwa Tarafa ya Ruhekei.