Unyanja FM

Serikali yazidi kuimarisha miundombinu ya barabara na maji Nyasa

October 31, 2023, 10:43 am

Serikali yazidi kuimarisha miundombinu ya barabara na maji Nyasa

Mkuu wa wilaya ya nyasa MH.FILBERTO HASSAN SANGA amewahasa wananchi  kutumia vizuri fursa za uchumi zinapojitokeza hasa  kilimo na uvuvi kwa kuwa ndio shughuli tegemezi na zinazofanywa na watu wengi wilayani humo

aliyasema hayo oktoba 27 katika ziara yake alipotembelea  kijiji cha lipingo kata ya lundo wilayani nyasa alipokuwa akipokea changamoto za wananchi wa kijiji hicho na wilaya kwa ujumla

katika hatua nyingine MH FILBERTO SANGA alisema serikali inaendelea na mikakati ya  kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na huduma za maji ili zimfike kila mwanachi na kuondokana na adha hiyo