Unyanja FM
Unyanja FM
October 14, 2025, 7:38 pm

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mwana wa Afrika, Bi. Rhoda Mwita Amesema kuwa Wakulima hawana budi kufanya kilimo Tija kwani hili ni hitaji kubwa hasa katika jamii nyingi nchini na ndiyo maana Wameamua kutoa mafunzo kwa Wakulima ili kuimarisha kilimo, kuinua kilimo sambamba na kuwajengea ushirikiano mzuri wakulima.
Taasisi ya Mwana Wa Afrika kwa kushirikiana na Uchumi Institute wamefanya mafunzo maalumu kwa Wakulima Wilaya ya Nyasa siku ya leo Oktoba 14 ambayo yamelenga kuwajengea wakulima hao uwezo kuhusu kilimo Tija, kanuni bora za kilimo, kuimarisha Ushirika na upatikanaji wa Masoko.
Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mwana wa Afrika, Bi. Rhoda Mwita Amesema kuwa Wakulima hawana budi kufanya kilimo Tija kwani hili ni hitaji kubwa hasa katika jamii nyingi nchini na ndiyo maana Wameamua kutoa mafunzo kwa Wakulima ili kuimarisha kilimo, kuinua kilimo sambamba na kuwajengea ushirikiano mzuri Wakulima.
Kwa upande wake, Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Nyasa Ndg. Pasifiki Mhapa Amekiri kuwa taasisi hiyo imekuwa msaada mkubwa kuwasaidia Wakulima kwani si mara ya kwanza kutoa Elimu na misaada hiyo hasa katika msimu huu ambao kilimo kimekaribia inawasaidia kujijengea uzoefu, uelewa na Weredi zaidi katika Shughuli hizo za Kilimo.

Aidha, Afisa Ushirika Wa Wilaya ya Nyasa Bw. Venance Ndomba Amesema kuwa Mafunzo wanayopata wakulima hao si tu kukuza kilimo bali kuinua maisha ya Mkulima Mmoja mmoja hivyo hawana budi kuyaishi na kuyatekeleza kwa Weredi.

Nae, Afisa Tawala Wilaya ya Nyasa, Mhe. Benedicto Nsindagi Wakati akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo amewaasa wakulima kuhakikisha wanatumia Elimu hiyo kunufaika zaidi katika kilimo.
“Mafunzo yoyote unayopata ujue kuwa Majukumu yanaongezeka” – Amesema
Kupitia kauli hiyo ameeleza kuwa anatarajia elimu waliyoipata inafungua Weredi, mikakati na itasaidia kukua zaidi katika kilimo hivyo amewataka Wakulima waliopata mafunzo hayo kuwa Walimu wazuri ili Migogoro ikapungue bali uzalishaji uongezeke zaidi

Hata hivyo, wakulima na viongozi wa Ambrose mbalimbali wamepongeza nankutoa ushuhuda kuwa Elimu wanayoipata pamoja na Mbolea zimekuwa msaada mkubwa huku wakiwaasa wasichoke kuwatembelea mara kwa mara katika Mafunzo wanayoyatoa.

Ikumbukwe kuwa, Mwana wa Afrika ni taasisi yenye vituo zaidi ya 18 katika kanda zote nchini ambapo inahusika na Usambazaji wa Mbolea, utoaji wa Elimu, sambamba na kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Uchumi Institute huku dhamira kuu ikiwa ni kuinua Sekta ya kilimo nchini sambamba na kuwainua Wakulima ili wawe na uwezo wa kufanya kilimo tija.