Unyanja FM
Unyanja FM
October 12, 2025, 9:48 am

Kujiandaa na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kwani hiyo ndio njia pekee ya kupata kiongozi bora na atakayefaa katika jamii.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyasa, Ndg Khalid Khalifa ameandaa Bonanza maalumu la watumishi Wilayani humo likilenga kuboresha Afya sambamba na kuhimiza kuhusu tukio la Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza na Unyanja Fm, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo katika Tukio hilo amesema kuwa lengo kuu ni kudumisha urafiki, undugu na umoja baina ya wananchi na watumishi kwa ujumla huku akiwaasa wananchi kujiandaa na kujitokeza kwa wingi siku a kupiga kura kwani hiyo ndio njia pekee ya kupata kiongozi bora na atakayefaa katika jamii.

picha na sauti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ya Nyasa Bw Khalid Kharifa
Kwa upande wake, Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo, Ndg Felister Nyome amesema kuwa huo ni muendelezo wa matukio ya aina hiyo Wilayani kwaajili ya kuimarisha ushirikiano baina ya watumishi, kuboresha afya pamoja na kulenga dhamira kuu ya kuwaunanisha watumishi wa idara mbalimbali pamoja na kuwakumbusha wananchi kuwa kuchagua kiongozi ni wajibu wa kila Mwananchi hivyo hawana budi kujitokeza kwa wingi siku ya tukio hilo la uchaguzi mkuu.
Sauti ya afisa utamaduni wilaya ya nyasa Ndg Felister Nyome
Nao, baadhi ya Watumishi wa Bonanza hilo wamefurahishwa na kupongeza Uongozi kwa kuandaa tukio hilo huku wakiomba iwe ni endelevu kwani linawasaidia kuboresha Afya, Kufahamiana zaidi sambamba na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani baina yao pamoja na watumishi wengine wa halmashauri hiyo.

Picha Hapo juu na Sauti ni washiriki wa bonanza la Watumishi Nyasa
Ikumbukwe kuwa tukio hilo limefanyika siku ya leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyasa likiwa na mjumuisho wa Michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Uimbaji, Kukimbia kwenye magunia, Kubeba yai kwa Kijiko, Mpira wa Kikapu, Netball na mengineyo huku Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Perres Magiri ambaye amewakilishwa na Mkurugenzi wa wilaya katika bonanza hilo pamoja na kukabidhi zawadi kwa washindi.