Unyanja FM
Unyanja FM
October 12, 2025, 9:26 am

picha ya jengo la Takukuru Nyasa
Akizungumza katika tukio hilo, Bw. Chalamila amewapongeza viongozi wote sambamba na wananchi kwa kusimamia zoezi la ujenzi mpaka linakamilika huku akiwaasa kuwa viongozi wa dini, vyama, wananchi waendelee kupiga vita rushwa kwa kuripoti matukio hayo sambamba na kutumia namba ya dharula 113 ili tufikie hatua ya azimio kuwa Tanzania bila rushwa inawezekana.
Ikiwa ni katika Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Takukuru Wilaya ya Nyasa mnamo Oktoba 11,2025 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Takukuru, Bw. Crispin Fransis Chalamila amewataka viongozi na Wananchi kutunza vema jengo hilo pamoja na vitendea kazi vyote ili vidumu na kutumika mda mrefu zaidi.
Akizungumza katika tukio hilo, Bw. Chalamila amewapongeza viongozi wote sambamba na wananchi kwa kusimamia zoezi la ujenzi mpaka linakamilika huku akiwaasa kuwa viongozi wa dini, vyama, wananchi waendelee kupiga vita rushwa kwa kuripoti matukio hayo sambamba na kutumia namba ya dharula 113 ili tufikie hatua ya azimio kuwa Tanzania bila rushwa inawezekana.
Bw. Chalamila ameongeza kuwa fedha iliyobaki wakati wa ujenzi inapaswa kutumika kumalizia ujenzi wa ofisi ya Mlinzi kwa wakati huku akiwakumbusha wananchi kushiriki na kujiandaa vema katika tukio la Uchaguzi mkuu litakalofanyika oktoba 29, mwaka huu.

Kwenye picha hapo juu pamoja na sauti Ni Mkurugenzi Takukuru Taifa Bw Chalamila
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Milk-Takukuru Dkt. Emmanuel Kiyabo ameishukuru menejiment ya takukuru kwa kutambua hitaji la kujenga majengo mapya yatakayosaidia kuboresha huduma za Takukuru katika jamii huku akiahidi kuendelea kuchapa kazi kwa weredi, uzalendo na umahiri mkubwa katika kupambana na kuzuia Rushwa nchini.
Sauti ya mkurugenzi wa milki Takukuru Dkt Emmanuel Kiyabo
Ikumbukwe kuwa, Uzinduzi wa jengo hilo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali sambamba na Watumishi mbalimbali ambapo ujenzi wa jengo hadi kukamilika umegharimu jumla ya Tsh, Milioni 307 katika awamu zote mbili huku matumizi yakitumia Tsh. Milioni 294 na baki ikiwa ni Milioni 12 ambayo imelenga kumalizia ujenzi wa kibanda cha mlinzi jambo linaloendelea kufanyiwa kazi ingawa mradi huo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ziliifanya kamati kutumia njia mbalimbali hadi kufanikiwa kukamilisha mradi huo.