Unyanja FM

Nyasa waaswa kuchangamkia fursa za bandari

September 17, 2025, 11:29 am

Ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ukiendelea ziwa Nyasa

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Perresi Magiri amewaasa wananchi wa Nyasa kuwa na tabia ya kuzichungulia fursa mbalimbali kwa kutazama changamoto zilizopo katika jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Perresi Magiri amewaasa wananchi wa Nyasa kuwa na tabia ya kuzichungulia fursa mbalimbali kwa kutazama changamoto zilizopo katika jamii.

Mkuu huyo amezungumza hayo katika kipindi maalum kilichofanyika katika Studio ya Unyanja FM hii leo ambapo ameeleza kuwa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi mkubwa wa Bandari wenye bajeti ya Tsh. Bilioni 80 ambapo ni mradi mkubwa utakaosaidia kutanua wigo wa Usafirishaji, Biashara ya Bidhaa mbalimbali hivyo Wananchi wanaweza tazama hitaji la soko, jamii na kisha kuanzisha fursa zitakazokuza uchumi badala ya kusubiri na kuagizwa bidhaa kutoka Msumbiji, Kariakoo na masoko mengine ile hali fursa inakuja nyumbani.

Kwenye picha ni Mkuu wa Wilaya ya nyasa Mh Perres Magili akiwa ndani ya studio za Unyanja FM

‎Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya amepongeza jitihada za Serikali katika kutekelezwa kwa miradi mbalimbali  ya maendeleo kwani wapo katika mpango mwingine mkubwa ambao ni kupata soko kubwa Wilayani Nyasa ambalo litasaidia kutanua wigo wa kibiashara katika jamii.