Unyanja FM

DC Nyasa: Mgombea urais CCM apokelewe kwa ‘vibe’

September 17, 2025, 11:05 am

kwenye picha ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Mh perres Magili

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mh. Perresi  Magiri amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mgombea nafasi ya Urais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza Mh. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi yatakayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mh. Perresi  Magiri amewaasa wananchi kujitokeza kwa Wingi katika mapokezi ya Mgombea nafasi ya Urais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassani pamoja na Mgombea Mwenza Mh. Balozi Emmanuel Nchimbi yatakayofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Kuelekea katika tukio hilo, Mgombea Mwenza wa Nafasi ya Urais Mh. Nchimbi atawasili Nyasa tarehe 20 mwezi huu wa tisa na ataanza kufanya kampeni kata ya Litui, Linga, Mbaha, Ngumbo, Liwindi na maeneo jirani hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo ambalo litaanza kuanzia majira ya Saa mbili asubuhi kisha ataelekea Mbambabay, Nyasa.

Aidha, Ziara ya Mgombea Mwenza inaenda sambamba na ujio wa Mgombea nafasi ya Urais Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan ambaye atawasili  tarehe 21 mwezi wa tisa Katika Wilaya ya Nyasa eneo la Mbambabey kwenye viwanja vya Bandari hivyo wananchi wameaswa kujitokeza kwa wingi wakiwa na vaibu katika tukio hilo ili kueleza changamoto, matatizo sambamba na kusikiliza sera mbalimbali za Wagombea hao kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

‎Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amemaliza k wa kueleza kuwa Ujio wa Mheshimiwa Rais ni fursa kubwa itakayosaidia kukamilika kwa Miradi kama Vile mradi wa Bandari wa Bilioni 80, Changamoto za Barabara na miradi mingine ya maendeleo hivyo siku mbili za ziara hiyo wamejipanga vizuri kusikiliza na kupokea ugeni huo utakaofanyika katika uwanja wa Mbambabey- Bandari ikisindikizwa na Burudani za Wasanii mbalimbali, Usikilizaji wa Sera za wagombea kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais kupitia chama Cha Mapinduzi.