Unyanja fm yapewa tahadhari kuelekea uchaguzi
April 20, 2024, 12:01 pm
Ruhundwa amesema vitendo vya upendeleo wakati wa kuwahoji viongozi au wanachama wa vyama vya siasa hususan nyakati za uchaguzi zinaweza kuleta chuki na kusababisha migogoro mikubwa na hata ugomvi kati ya Waandishi au watoa maadhui na wanasiasa au wafuasi wa vyama.
picha ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka unyanja fm na mwl wa mafunzo Hilary Luhundwa
Watoa maudhui redioni na Mtandaoni wa Unyanja FM, wametahadharishwa dhidi ya habari za zinazotoa upendeleo kwa Vyama vya siasa ili kujiepusha na migogoro wakati wa uchaguzi.
Tahadhari hiyo imetolewa na Hilary Ruhundwa mhariri wa Redio TADIO, wakati wa mafunzo ya upakiaji wa maudhui mtanadaoni, yanayotolewa na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania-TADIO kwa redio wanachama
Ruhundwa amesema vitendo vya upendeleo wakati wa kuwahoji viongozi au wanachama wa vyama vya siasa hususan nyakati za uchaguzi zinaweza kuleta chuki na kusababisha migogoro mikubwa na hata ugomvi kati ya Waandishi au watoa maadhui na wanasiasa au wafuasi wa vyama.
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Kituo cha Redio Unyanja kilichopo Nangombo Wilayani Nyasa ambayo ni mwanachama-TADIO, yamelenga kuwajengea uwezo waandishi habari kuhusu uwekaji maudhui mtandaoni,Maadili na utafutaji wa masoko ya biashara kidijiti.
na patrick kossima