Savvy FM
Savvy FM
26/02/2026, 22:56

Wasimamizi na watendaji wa taasisi zilizopo katika sekta ya viwanda na biashara wametakiwa kuondoa urasimu na kuwa wawezeshaji wa sekta binafsi, kuchochea shughuli za uzalishaji, masoko ya kimkakati na uchumi kwa maendeleo endelevu ya kisekta kwa Taifa.
Na Mariam Mallya
Katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara, Balozi Waziri Salum, amesisitiza hilo akiwa jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi chake na Wakuu wa taasisi hiyo na kusisitiza uwajibikaji kwa wasimamizi waliopo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya viwanda na biashara ili kuongeza tija kwa maslahi ya Taifa.
Naibu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara Aristides Mbwasi amesema sekta ya viwanda na biashara ni msingi wa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi hivyo sekta hiyo haina budi kubeba jukumu la kupambana kutafuta masuluhusho ya changamoto mpya ili kufikia malengo ya dira ya 2050.