Savvy FM
Savvy FM
February 24, 2026, 11:16 pm

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda, amesema jiji la arusha linaendelea kunufaika na fedha za maendeleo zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha miundombinu na huduma za kijamii
Na Mariam Mallya
Akizungumza mapema leo katika ziara ya waziri mkuu ya kukagua miradi ya maendeleo ameeleza kuwa jiji la arusha linaenda kupendezeshwa na barabara za njia nne zenye kiwango huku akisema Arusha ni moja ya mikoa wenyeji wa mashindano ya Afcon 2027 hivyo kabla ya mashindano hayo tayari kutakuwa na mabasi ya mwendo kasi.
Naye Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameonyesha kuridhishwa na kasi na ubora wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo jijini Arusha, ikiwemo ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Bondeni City Bus Terminal na Soko la Kilombero, akisisitiza uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma kwa ajili ya kuboresha mazingira ya biashara kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa soko jipya la Kilombero ametoa maelekezo mara tuu soko hilo litakapokamilika kipaumbele kiwe wale waliokuwa wanafanya biashara katika eneo hilo huku akitoa onyo kwa baadhi ya watu wanaofanya ulanguzi kwa kushika eneo na kisha kulipangisha kwa bei kubwa kwa wafanya biashara