Savvy FM

Uzinduzi mradi wa pikipiki wainua uchumi wa vijana Arusha

January 14, 2026, 5:08 pm

Joseph Mkude,mkuu wa Wilaya ya Arusha akiwa kwenye uzinduzi wa mradi.Picha na Mariam Malya

Zaidi ya vijana 200 jijini Arusha wameanza kunufaika na mradi wa kuwawezesha kiuchumi kupitia mpango wa kukopeshana pikipiki kwa gharama nafuu, uliozinduliwa na Umoja wa Maafisa Usafirishaji jijini Arusha kwa kushirikiana na kampuni ya TVS (Trust Value Service), lengo likiwa ni kuongeza ajira, kipato na ustawi wa vijana wanaojishughulisha na usafirishaji wa pikipiki.

Na Mariam Malya

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Katibu wa Boda Boda Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Magembe, kwa niaba ya maafisa usafirishaji amesema mradi huo umeanza kuwanufaisha wanachama 200, ambapo pikipiki hizo zimetolewa kwa mfumo wa kukopeshana kwa masharti nafuu. Amesema pikipiki hizo ni za majaribio zilizoanza kutumika mapema mwezi Desemba mwaka jana, hatua inayolenga kupima ufanisi wa mradi kabla ya kuupanua zaidi.

Sauti Richard Magembe,Katibu wa Boda Boda Mkoa wa Arusha

Akikabidhi rasmi pikipiki hizo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Modest Mkude, amewataka maafisa usafirishaji kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya hususan wakati wa ajali. Mhe. Mkude pia amejitolea kuchangia vikundi 10 vyenye watu sita sita, endapo mfumo wa bima ya afya utaruhusu kusajili watu hao kutoka vikundi tofauti.

Sauti ya Joseph Mkude Mkuu wa Wilaya ya Arusha

‎Kw upande wa jeshi la polisi inspecta mzirai usalama wa barabarani amesema wamepokea maelekezo yote ya mkuu wa wilaya wataenda kuzifania kazi ‎

Sauti ya inspecta mzirai afisa usalama wa barabarani Mkoa wa Arusha