Savvy FM
Savvy FM
October 22, 2025, 11:15 pm

Mafundi Gereji zaidi ya 200 Krokoni Waeleza Kero Zao kwa Mkuu wa Wilaya Arusha, DC Mkude Aahidi Utekelezaji na Onyo kwa Wanaotumia Trampa
Na Jenipha Lazaro
Umoja wa Mafundi gereji Krokoni mtaa wa Kitangare, kata ya Kimandolu mkoani Arusha wamemuomba mkuu wa wilaya kuweza kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwemo ajira, barabara, kutoa vibali kwa mafundi gereji pamoja na madereva bodaboda wanaoweka trampa.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude ambaye ametembelea eneo hilo kusikiliza kero ya mafundi hao, ameweza kutolea ufafanuzi juu ya changamoto zilizoelezwa na kusema tatizo la kutokupewa mikopo, amesema atamuelekeza mtaalamu aje kuwaunganisha umoja wao na kuangalia mikataba ili waweze kupata mikopo ya halmashauri au taasisi zinazotoa mikopo.