Savvy FM

Maadhimisho elimu ya watu wazima, nje ya mfumo rasmi yafana Arusha

October 4, 2025, 9:01 pm

Picha ya Wanafunzi wa elimu ya watu wazima.Picha na Jenipha Lazaro

Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya watu wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yamefanyika leo, Jumamosi tarehe 04 Oktoba 2025, katika viwanja vya Shule ya Msingi Levolosi, Wilaya ya Arusha. Maadhimisho haya yamekusanya washiriki mbalimbali wakiwemo walimu, wanafunzi wa elimu ya watu wazima, wadau wa elimu, pamoja na viongozi wa serikali kwa lengo la kuhamasisha umuhimu wa elimu endelevu kwa watu wa rika zote, hasa wale waliokosa fursa ya kujiunga na mfumo rasmi wa elimu wakiwa katika umri mdogo.

Na Jenipha Lazaro

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, ambaye aliwakilishwa na Afisa Tarafa Bi. Chausiku. Katika hotuba yake, Bi. Chausiku alisisitiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki ya msingi ya elimu, bila kujali umri au mazingira aliyopitia.

Sauti ya Bi Chausiku,Afisa Tarafa

Kwa upande wake, Afisa Elimu wa watu wazima Mkoa wa Arusha, Bw. Emanuel Mahundo, alisema kuwa lengo la mpango huo ni kuhakikisha kila mmoja ananufaika na elimu hiyo, bila kubaguliwa.

Sauti ya Emanuel Mahundo, Afisa Elimu watu wazima Mkoa wa Arusha

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa elimu ya watu wazima, Jack Sebastian alieleza namna alivyojikuta akikumbwa na changamoto ya ujauzito akiwa bado mwanafunzi wa shule ya sekondari, hali iliyosababisha ndoto zake kukatizwa.

Sauti ya Jack Sebastian,mwanafunzi elimu ya watu wazima