Savvy FM

Ghasia mtaa wa Arc: Polisi wamdaka mama anayetuhumiwa kuvuruga amani

September 26, 2025, 11:43 pm

Wananchi wa mtaa wa Arc wakijadiliana jambo.Picha na Jenipha Lazaro

Hali ya taharuki imetanda katika Mtaa wa Arc, Kata ya Oloirien, jijini Arusha, baada ya wananchi kuandamana wakipinga vitendo vya kile wanachodai ni ‘kubambikiziwa kesi’ na mama mmoja anayefahamika kwa jina la ‘Mchinaaa’, ambaye ni mmiliki wa baa maarufu katika eneo hilo.‎

Na Jenipha Lazaro

Kwa mujibu wa wananchi waliokusanyika kwa hasira, wamedai kuwa wamechoshwa na tabia ya mama huyo kuwasingizia makosa mbalimbali, ikiwemo madai ya kubakwa kwa mtoto wake, pamoja na kudai bili kubwa za vinywaji wanapohudhuria katika baa yake.‎

Sauti ya Wananchi wa mtaa wa Arc

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Mtaa wa Arc, Bw. Benedict Kavishe, amesema ofisi yake tayari inashughulikia jumla ya kesi tano zinazomuhusu mama huyo. Kwa mujibu wa Kavishe, hali hiyo imeilazimu Serikali ya Mtaa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuchukua hatua za kiusalama.‎

Sauti ya bw.Benedict Kavishe,Mwenyekiti wa Mtaa wa Arc