Savvy FM

BAKWATA Arusha yatoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum

September 25, 2025, 7:05 pm

Viongozi wa BAKWATA Arusha.Picha na Jenipha Lazaro

Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Arusha umetembelea na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika shule ya msingi Kaloleni, inayowahudumia watoto wenye mahitaji maalum, kama sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Maulid yatakayofanyika Jumamosi hii jijini Arusha.

Na Jenipha Lazaro

Msafara huo uliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Shabani Juma, akiwa ameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Arusha, Hussein Ijunje, pamoja na Katibu wa JUAKITA, Tausi Swalehe.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo, viongozi hao walisema kuwa kitendo cha kuwaonea huruma na kuwahudumia watu wenye uhitaji ni wajibu wa kila mwanajamii.

Sheikh Shabani Juma alieleza kuwa watoto wenye mahitaji maalum wanahitaji mazingira bora ili waweze kupata elimu sawa kama watoto wengine, na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia shule hiyo.

Sauti ya Shabani Juma,Sheikh Mkoa wa Arusha.

Kwa upande wa uongozi wa shule, Mwalimu Mkuu Miminini Payema, Mwalimu wa kitengo maalum pamoja na Sarah Makange, waliishukuru BAKWATA kwa msaada huo, huku wakielezea changamoto kubwa inayowakabili — hususani usafiri wa wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali.

Sauti ya Walimu wa shule ya Kaloleni