Savvy FM
Savvy FM
September 3, 2025, 2:47 pm

Kampuni ya Mati Super Brands Ltd kupitia kampuni tanzu Mati Technologies imekuja na teknolojia ya kisasa ya Ndege nyuki (drone) kwa ajili ya sekta ya kilimo na huduma nyingine za kijamii ili kuongeza ufanisi.
Na Mussa Kinkaya
Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Group of Companies David Mulokozi, amesema kampuni hiyo imeamua kuwekeza kwenye teknolojia ya drone zitakazotumika kunyunyizia dawa mashambani, kupima maeneo, kupanda mbegu, kusafirisha mizigo, kusaidia kaguzi mbalimbali
Katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaji, amesema mkoa wa Manyara utakuwa wa kwanza kwa Afrika kuwa na kiwanda cha drone hali itakayopandisha hadhi ya mkoa.
Afisa Ushirika kutoka ofisi ya msajili mkoa wa Manyara, Godamen Merinyo, amesema teknolojia hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wakulima, hususan katika mazao kama mbaazi ambayo mara nyingi hukua kwa urefu na kufanya upuliziaji wa dawa kuwa ngumu na wa gharama kubwa.