Savvy FM

Wananchi Osunyai walia na taka kutupwa kwenye mto Burka

September 1, 2025, 3:54 pm

Takataka zikielea mto Burka.Picha na Jenipha Lazaro

Wananchi waishio katika mtaa wa Kiriki A, kata ya Olsunyai, mtaa wa JR, jijini Arusha, wameiomba serikali na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kudhibiti utupaji wa taka hovyo kwenye mto Burka, wakieleza kuwa hali hiyo ni hatarishi kwa afya na huenda ikasababisha mlipuko wa magonjwa.

Na Jenipha Lazaro

Wakizungumza katika eneo la mto huo, baadhi ya wakazi hao wamesema kuwa taka zinazotupwa kwenye mto ni pamoja na pampers za watoto na watu wazima, mabaki ya vyakula, matunda na mazao mbalimbali, hali ambayo wamesema ni hatari kwa ustawi wa afya ya jamii.

Sauti wananchi wa Kata ya Olsunyai

Aidha, balozi msaidizi wa eneo hilo, bw. Ahmed Yusuph, amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuhamasisha usafi, lakini bado hazijazaa matunda. Ameongeza kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua kali zaidi ili kuzuia athari kubwa zinazoweza kujitokeza endapo hali hiyo itaendelea.

Sauti ya Ahmed Yusuph,balozi msaidizi mtaa wa Kiriri A