Savvy FM

Jamii zatakiwa kuthamini haki za Punda kama wanyama kazi

August 28, 2025, 5:39 pm

Wanyama aina ya Punda wakiwa kwenye malisho ya maji.Picha na Jenipha Lazaro

Jamii za kifugaji zimetakiwa kuwathamini wanyama kazi hususani mnyama punda, ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana potofu zinazowanyima haki zao kama vile uchinjaji holela, kuwabebesha mizigo kupita kiasi, pamoja na kutowapatia huduma za afya na ustawi wa jumla.

Na Jenipha Lazaro.

Wito huo umetolewa na wataalamu wa mifugo kutoka shirika lisilo la kiserikali la ASPA (Arusha Society for the Protection of Animals) linalojihusisha na ustawi wa wanyama, wakati wa zoezi la utoaji wa huduma za matibabu kwa wanyama katika soko la Mirongoine, kata ya Oljoro jijini Arusha.

Sauti ya Diana Msemo – Afisa Elimu Ustawi wa Wanyama, ASPA na Albert Mbwambo – Mtaalamu wa Wanyama

Aidha, baadhi ya wananchi wanaofuga na kutumia punda wameelezea mabadiliko chanya waliyoyapata baada ya kupata elimu ya ustawi wa punda. Wamepongeza jitihada za utoaji wa huduma za afya kwa wanyama hao, wakisema zimewaokoa punda wao na kuongeza tija kiuchumi. Wamekemea vikali ukatili dhidi ya wanyama hao.

Sauti ya Meng’oriki Kispan na Namnyaki Kiki-wafugaji wa Punda