Savvy FM

Wananchi watakiwa kukata bima kujilinda na majanga

August 9, 2025, 10:03 am

Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima, Bwa. Bahati Ogolla akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Jenipha Lazaro

Jamii imetakiwa kuhakikisha inakata bima kwa shughuli mbalimbali za kila siku, ili kujilinda dhidi ya majanga yasiyotegemewa yanayoweza kuathiri maisha yao ya kijamii na kiuchumi.

Na Jenipha Lazaro

Wito huo umetolewa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima, Bwa. Bahati Ogolla, wakati wa Maadhimisho ya 31 ya Sikukuu ya wakulima Nanenane – kwa Kanda ya Kaskazini yanayofanyika jijini Arusha, yakihusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.‎‎

Bw.Bahati amesema kuwa huduma za bima ni muhimu kwa wananchi wote, kwani zinawasaidia kujikinga na hasara au gharama kubwa zinazoweza kutokea pindi wanapopatwa na majanga kama moto, ajali, vifo au uharibifu wa mali.‎

Sauti ya Meneja wa Kanda ya Kaskazini kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima, Bwa. Bahati Ogolla

Katika hatua nyingine, Afisa Kodi Mwandamizi Nicodemus Massawe kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia ofisi yake ya mkoa wa Arusha, imetangaza kuwa kwa sasa huduma nyingi za ulipaji kodi na usajili wa vyombo vya moto zimehamia katika mifumo ya TEHAMA ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa walipakodi na kupunguza msongamano katika ofisi za serikali.‎‎

Sauti ya Afisa Kodi Mwandamizi Nicodemus Massawe