Savvy FM

Kanda ya Kaskazini waalikwa maonesho ya nishati safi nanenane

July 29, 2025, 7:16 pm

Kenani Kihongosi,Mkuu wa Mkoa Arusha.Picha na Msukuma

Kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Kihongosi, amewaalika wananchi wote wa mkoa huu pamoja na mikoa jirani kushiriki katika maonesho ya teknolojia ya nishati safi.

Na Jenipha Lazaro

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mhe. Kihongosi amesema maonesho hayo yatatoa elimu juu ya matumizi salama ya nishati safi ya kupikia na athari za kiafya na kimazingira zitokanazo na matumizi ya nishati isiyo salama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Bi Noren Mawala, amesema ni muhimu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufungua fikra zao kuhusu mabadiliko ya nishati kuelekea matumizi endelevu.