Savvy FM

Washiriki 86 wapatiwa mafunzo ya uchaguzi Arusha

July 22, 2025, 2:15 pm

Washiriki wa mafunzo ya uchaguzi yaliyotolewa jijini Arusha. Picha na Jenipha Lazaro

Washiriki 86 kutoka mikoa ya Arusha na Manyara  wamepatiwa mafunzo ya uchaguzi yakilenga kuwaanda kusimamia mchakato wa uchaguzi kwa weledi.

Na Jenipha Lazaro

Mjumbe wa tume ya uchaguzi nchini Zakia Abubakar amesema masharti ya ibara ya 74 ya ibara  ndogo ya 6 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 tume huru ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kusimamia uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, wabunge  na madiwani kwa Tanzania bara.

‎Zakia ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uchaguzi yaliyoandaliwa na Tume huru ya uchaguzi nchini jijini Arusha ambapo amesema wasimamizi wa ngazi za kata wameteuliwa kwa mujibu washeria hivyo wanawajibu kikatiba na kisheria kusimamia na kuratibu uchaguzi kwa niaba ya tume huru ya uchaguzi katika  maeneo yao ya uteuzi

Sauti ya Mjumbe wa tume ya uchaguzi, Zakia Abubakar

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi  Jafar Makupula  amesema kuwa Tume imeendelea na mafunzo ya mchakato wa uchaguzi kwa waratibu wa uchaguzi ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia uchaguzi  kwa watendaji waliochaguliwa kuratibu zoezi hilo.

Kaimu Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi  Jafar Makupula

Kauli mbiu ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 inasema; kura yako haki yako jitokeze kupiga kura .